KAPOMBE AANZA KUIONA TAMU YA KUCHEZA SOKA ULAYA
Hatimaye nyota na beki mahiri wa kimataifa wa tanzania SHOMARI KAPOMBE aanza kunyookewa na mambo baada ya hapo juzi kupiga picha na moja kati ya mabeki mahiri alietamba katika soka la ulaya WILLIUM GALLAS aliyengara na vilabu kama Chelsea, Arsenal an Tottenham Spurs za Uingereza na sasa ameamua kurudi nyumbani kufanya mazoezi na clab ya AS Cannes. Kapombe mwenyewe amefurahishwa na hatua hiyo huku akisema atajifunza mambo mengi sana kutoka kwa beki huyo wa kati wa zamani wa timu ya taifa ya UFARANSA "Imekuwa ni faraja kwangu kukutana mtu kama Willium Galllas na kubwa zaidi kufanya nae mazoezi natumaini ntajifunza mambo mengi kutoka kwa mchhezaji huyu kutokana na uzoefu wake," Kwa upande mwingine Gallas ameelezea kufurahiswa na kiwango cha nyota huyo wa zamani wa simba na kusema kuwa atakuja kuwa moja kati ya malinzi mahiri duniani kama ataendelea na juudi alizonazo
"Actually i have been impressed by his performance, and i think he may become a great player if he keeps on his effort. He is a good player general "
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni