Jumanne, 26 Novemba 2013
WAJUE WANASOKA WATANO MAHIRI ZAIDI AMBAO WANA NAFASI KUBWA YA KUTWAA UCHEZAJI BORA WA BBC 2013/2014
WASIFU WAKE: Victor Moses ni mchezaji mwenye umri wa
miaka 22, ambaye kwa sasa anachezea klabu yake ya nne ya Liverpool huko
England baada ya kuhama kwa mkopo kutoka klabu ya Chelsea jambo
linalomweka kwenye mtihani wa kama ataweza kufurahia kiwango chake au
atashindwa kudhihirisha kiwango chake.
Victor Moses ni raia wa Nigeria ambaye ana kila sifa ya kuchangia mafanikio makubwa kwenye timu. Ana kasi, ana uwezo wa kufunga magoli, ana uwezo wa kucheza nafasi tofauti uwanjani kutoka nafasi ya kiungo hadi ushambuliaji. Moses alionja ladha ya kuchezea vilabu vikubwa katika ligi kuu ya England wakati alipojiunga na Crystal Palace klabu aliyoicheza klabu hiyo uanzia mwaka 2007 hadi mwaka 2010 na kufanikiwa kufunga magoli 11 katika mechi 58 alizocheza kabla ya kuhamia klabu ya Wigan Athletic. Katika miaka miwili akiwa Wigan, Victor Moses alifanikiwa kupachika wavuni magoli nane katika mechi 74 alizocheza.
Mwezi Agosti mwaka 2012, Moses alirudi tena London baada ya kununuliwa na Chelsea kutoka Wigan kwa uhamisho wa Paundi million 9. Hata hivyo baadae Kocha Jose Mourinho ambaye alirudi kufundisha Chelsea kwa mara ya pili hakumweka Moses katika orodha ya wachezaji ambao ni chaguo lake. Kwa sasa Moses amehamia Liverpool tangu mwezi Septemba mwaka huu kwa mkopo wa muda mrefu. Akiwa Liverpool makali yake yameanza kuonekana ambapo katika mechi yake ya kwanza kwenye klabu hiyo alifunga bao pale timu hiyo ilipokutana na Swansea. Moses ameshacheza mechi zaidi ya saba akiwa Liverpool na anaonekana kuwa ni miongoni mwa wachezaji tegemeo walioifanya Liverpool ianze ligi kuu ya England kwa kishindo. Kwa upande wa ngazi ya kimataifa Moses anachezea timu ya taifa ya Nigeria japokuwa alishawahi kuichezea England katika timu ya vijana hadi walio chini ya miaka 21. Victor Moses ni miongoni mwa wachezaji wa timu ya taifa ya Nigeria walioiwezesha kutwaa kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013.
Wadadisi wana maoni gani kumhusu Victor Moses?
Waandishi na wachambuzi wanamwelezea Victor Moses ni mmoja wa wachezaji ambao wamekuwa hawapangwi kuanza kila mechi kwenye klabu yake au anapocheza timu ya taifa hii ni kwa lengo la kuongeza nguvu kwa wale wanaokuwa wanacheza. Amekuwa akifurahia kila anapopewa nafasi uwanjani na hii imejidhihirisha kwa kazi yake anapokuwa uwanjani. Pamoja na uwezo, uimara na shauku yake anapokuwa uwanjani Moses ni mshambuliaji ambaye anaweza kucheza nafasi yoyote na zaidi ya hayo amekuwa akifunga magoli muhimu na kwa wakati muhimu. Mara chache amekuwa akitumiwa kama kiungo mchezeshaji lakini hufurahia zaidi anapochezeshwa kama mshumbuliaji ya nyuma.Chelsea na Nigeria zinapaswa kumshukuru Moses kwa kuzisaidia timu zao kuchukua makombe muhimu mwaka 2013. Kwa upande Chelsea Moses alifunga magoli muhimu siku ya roba fainali na nusu fainali ya ligi ya Europa ambapo baadae Chelsea ilinyakua kombe hilo. Katika timu ya taifa ya Nigeria kwenye Fainali za kombe la Mataifa ya Afrika Victor Moses alikuwa ni miongoni mwa wachezaji muhimu walioiwezesha kunyakua kombe hilo na alishiriki kupiga mikwaju ya penati muhimu za mwisho. Umuhimu wake kwenye timu ya taifa unajidhirisha kwa kuteuliwa kwenye orodha ya wachezaji wanaounda kikosi cha timu hiyo japo amekosa mechi kadhaa za kufuzu kombe la dunia. Kwa ujumla kwa mwaka mzima Moses amekuwa akikabiliwa na majeraha na kufanya akose baadhi ya mechi za kimataifa kwenye timu yake ya Nigeria. Mbali na hayo kwa sasa Moses amejidhihirisha kuwa ni mmoja ya wachezaji muhimu katika kikosi cha Liverpool tangu alipojiunga na timu hiyo msimu huu wa ligi kuu ya England ambapo alifunga goli katika mechi ya kwanza wakati Liverpool ilipocheza na Swansea. Akiwa pamoja na Luis Suarez na Daniel Sturridge ambao ni washambujiaji tegemeo wa Liverpool Moses amekuwa akipangwa ili kuwasaidia kama mshambuliaji anayewatengenezea nafasi.Akiwa mchezaji wa timu ya Chelsea ya England kwa miaka saba, John Mikel Obi amecheza mechi 187 na kushinda makombe kadhaa, likiwemo la ubingwa wa Ligi Kuu ya England, Kombe la Mabingwa barani Ulaya na makombe manne ya chama cha mpira cha England, FA. Angaliweza kuwa mchezaji wa Manchester United, wakati huo klabu hiyo ya Old Trafford walifikiri wangemsajili mchezaji huyo kutoka klabu ya Lyn Oslo ya nchini Norway wakati huo John Mikel akiwa na umri wa miaka 18. Hata hivyo, baada ya mvutano kuhusu suala lake, hatimaye klabu ya Chelsea ikafanikiwa kumsajili mchezaji huyo kinda mwezi Juni 2006. Tangu wakati huo, Mikel hajaweza kukengeuka kuhusu timu yake na hivyo kujijengea uwepo wake wa mara kwa mara katika kikosi cha Chelesea the Blues na kikosi cha taifa cha Nigeria-kwa kuichezea nchi yake mara 51 na kusaidia kuipatia ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika mapema mwaka huu. Mikel ni mchezaji mzuri katika nafasi ya kiungo na mwenye nidhamu awapo mchezoni, na ilimchukua Mikel hadi mwezi Septemba mwaka huu kufunga bao lake la kwanza kwa timu yake ya Chelsea katika Ligi Kuu ya England, akiichezea timu hiyo mara 185, katika mechi hiyo Chelesea ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fulham. Labda kiwango chake cha juu kabisa alikionyesha mwaka 2012 katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bayern Munich, ambapo Mikel alionyesha mchezo wa kiwango cha juu katika nafasi ya kiungo mlinzi na kusaidia timu yake kupata sare ya 1-1 baada ya dakika 120 za mchezo mkali uliomilikiwa na miamba hiyo ya Ujerumani. Chelsea waliendelea kupigana na kuingia katika hatua ya mikwaju ya penalti. Na ndipo waliposhinda na kunyakua kombe hilo, wakiwa chini ya uongozi wa kocha Roberto Dimateo. Umuhimu wa Mikel katika kikosi cha Chelsea ni kwamba mwaka jana aliongeza mkataba wa miaka mitano kuicheza klabu hiyo, hivyo kumaanisha atakuwepo Stamford Bridge hadi mwaka 2017.
Tathmini kumhusu Obi Mikel ?
Baada ya Nigeria kutwaa ubingwa mwaka 2013, huu umekuwa mwaka ambao John Mikel Obi amedhihirisha kuwa mmoja wa wachezaji mahiri kabisa barani Afrika. Hakuna mchezaji yeyote barani Afrika ambaye amepata mafanikio makubwa mwaka huu kama mchezaji huyu wa Nigeria, ambaye aliuanza msimu huu kwa mafanikio makubwa na kwenda mbele zaidi. Kufanikiwa kwa Mikel katika kusakata kandanda kumekuwa na mwelekeo mzuri lakini pia akikabiliana na changamoto kadha. Miaka mingi ya kucheza nafasi ya ulinzi katika klabu yake ya Chelsea, kumepunguza kasi yake ya kuwa mchezaji mshambuliaji katika timu yake ya taifa ya Super Eagles. Ufanisi wake katika timu ya Nigeria katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika za mwaka 2013, kulienda mbali zaidi kuwakumbusha mashabiki mchango wake katika nafasi ya ulinzi. Katika mashindano yaliyofanyika Afrika Kusini, alikuwa mmoja wa wachezaji wakongwe wa klabu hiyo, akiwa na umri wa miaka 25 tu na kupewa majukumu ya kuwa mshambuliaji kiungo tofauti na nafasi ya kiungo mlinzi anayochezea katika klabu yake ya Chelsea. Nigeria ilishinda Kombe la Mataifa ya Afrika, Mikel akiwa mchezaji katika mecho zote. Nigeria, Super Eagles waliwalaza Burkina Faso bao 1-0 katika mchezo wa fainali.Matunda ya mwanasoka Jonarthan Pitroipa kuibuka kuwa mmoja wa watakao wania tuzo ya BBC yalionekana hasa baada ya kuanza kwa michuano ya kombe la mataifa barani Afrika, ambapo Burkina Faso ilipangwa katika kundi gumu likiwa na Timu ya Zambia na Nigeria. Si tu walifanikiwa kuing’oa Chipolopolo, mabingwa watetezi, pia waliongoza kundi hilo wakiwa mbele ya Nigeria. Super Eagles ilifanya jitihada za kuishinda Burkinabe katika mchuano wa fainali, mwishowe hakuna mchezaji mwingine yeyote wa Nigeria isipokuwa Pitroipa wa Burkinafaso aliyechaguliwa kuwa mchezaji bora kwenye michuano hiyo. Winga huyo kutoka klabu ya Rennes amekuwa chachu ya kufanya vizuri, akisawazisha bao dakika za mwisho katika mpambano wa ufunguzi na mchuano uliofuata akifunga bao moja na kutengeneza mawili wakati timu yake ilipokuwa ikicheza huku wakiwa kumi na kuibuka washindi wa mabao 4-0 Huo ulikuwa ushindi wa kwanza wa Stallion katika michuano ya kombe la mataifa barani Afrika tangu iliposhika nafasi ya nne mwaka 1998 timu hiyo ilipokuwa mwenyeji wa mashindano ambapo Pitroipa aliisaidia timu yake kuingia kwenye raundi ya nusu fainali alipoifungia timu yake bao 1-0 wakati wa muda wa nyongeza walipochuana na Togo. Pitroipa aliondolewa kimakosa kwa adhabu ya kadi nyekundu kwenye hatua ya nusu fainali timu yake ilipocheza na Ghana , Nyota huyo wa zamani wa Hamburg hatimae alicheza mchezo wa fainali baada ya adhabu ya kadi nyekundu kutenguliwa, hata hivyo Burkinafaso ilipoteza mchezo huo kwa kufungwa goli 1-0. Hakuna mchezaji yeyote wa Burkinafaso aliyefikia hatua ya kushinda tuzo ya BBC ya mchezaji bora wa Afrika wa mpira wa miguu wa mwaka , lakini Jonathan Pitroipa anastahili.
Kwa wengi anajulikana na kukubalika kama mmoja wa Viungo bora katika kizazi cha sasa cha wanasoka.Yaya Toure ni roho ya Timu huku akitawala na kuheshimika pande zote. Mwanasoka huyu alijiunga na Klabu yake ya sasa ya Manchester City mwaka 2010 na tangu wakati huo ameshinda Taji la Ubingwa wa Ligi kuu ya Kandanda England likiwa ni taji la kwanza kwa Timu hiyo katika miaka 44,vile vile Kombe la FA,na pia ngao ya Jamii kwa Mabingwa hao wanaovalia Jezi ya Blue ya mawingu. Toure ambaye tayari ameishacheza zaidi ya mechi 109 kwenye klabu hiyo na kufunga magoli 23,yakiwemo magoli ya rekodi yatokanayo na Mipira ya adhabu,na ameendelea kuwa mmoja wa wachezaji muhimu katika klabu hiyo. Alijunga na Manchester City akitokea Barcelona ambako alikaa kwa miaka mitatu huku akitwaa mataji kadhaa ikiwa ni pamoja na Ubingwa wa Ligi kuu ya Spain mara mbili,Ubingwa wa Ulaya mara moja,Na Kombe la Super Cup na pia taji la klabu bingwa ya Dunia.Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 vile vile amekwishatwaa Ubingwa wa Soka huko Ugiriki akiwa na Klabu ya Olympiacos,na pia Ubingwa wa Ligi kuu katika nchi yake ya asili Ivory Coast.Jambo la Kusikitisha kwa Yaya Toure ni katika medani ya kimataifa ambapo kizazi cha wanasoka kinachoaminika kuwa kizazi cha dhahabu katika soka la Ivory Coast kimeshindwa kutwaa Kombe ambalo limekuwa likitarajiwa kutoka kwao.Kwa kufungwa na Zambia mwaka 2012 katika Mechi ya Fainali ya Kombe la Mataifa yalikuwa matokeo yaliyoleta mshtuko katika Soka Barani Afrika.Hata sasa akiwa na umri wa miaka 30 Yaya Tore bado hajaonyesha dalili za kushuka kiwango ambapo ameanza vema msimu huu wa soka akiwa na Klabu yake na Manchester City ambapo hadi sasa amekwishatia nyavuni bao 7.huku akiendelea kuonyesha kiwango cha juu cha Ubora.Akiwa amekwishatwaa mara mbili taji la Mwanasoka bora wa mwaka wa Shirikisho la sokak barani Afrika CAF, Yaya Toure vile vile ni Mwanasoka pekee kutoka Barani Afrika kwenye orodha ya wachezaji 23 waliiorodheshwa kuwania tuzo ya Mwanasoka bora wa mwaka wa Shirikisho la Soka Duniani FIFA mwaka huu 2013.
WADADISI WASEMAJE KUMHUSU TOURE?
Ian Hughes ,ambaye ni Mwandishi wa Habari za Michezo wa BBC anasema kuwa msimu wa mwaka 2013 unaweza ukawa si mzuri kwa Yaya Toure kwa Upande wa Mataji,lakini bado Mwanasoka wa kimataifa wa Ivory Coast,ameonyesha kasi, Nguvu,ubunifu,Magoli ya Kufunga,na hata Uongozi.
Akiwa mchezaji wa zamani wa timu ya vijana ya AC MILAN, soka la Pierre Emerick Aubameyang lilianza kuchomoza baada ya kujiunga na klabu ya Saint Etienne kwa mkataba wa kudumu mnamo mwaka 2011.Lakini mkataba huo ulimalizika Julai baada ya kujiunga na washindi wa pili wa Kombe la Klabu Bingwa Barani Ulaya, Borussia Dortmund , akichukua nafasi ya Mario Gotze, baada ya uhamisho wake uliotarajiwa sana kwenda Bayern Munich.Lakini mkataba wake na Les Verts ulimalizika kwa mtindo wa aina yake, kwani kalbu hiyo ilishinda taji la French League One kwa mwaka 2013, hivyo kumwezesha Aubameyang , kupata tuzo yake ya kwanza kama mchezaji wa kulipwa.Ingawa hakufunga goli katika mchezo huo, lakini aliwahi kuzifumania nyavy mara 19, katika ligi kuu ya Ufaransa , huku mchezaji wa PSG, Zlatan Ibrahmovic, akiongoza kwa mabao, na mchezaji huyo kutoka Gabon akiwa ametoa pasi nane zilizozaa mabao.Uchezaji huo mahiri ndio ulioishawishi Dortmund, kumnunua kwa kitita cha Paundi milioni 11 kwa mkataba wa miaka mitanoNa mara alijiongezea tuzo, baada ya Dortmund kulipiza kisasi cha kufungwa katika fainali ya Klabu Bingwa Barani Ulaya jijini London mnamo Mei, kwa kuwafunga mahasimu wao Bayern Munich mabao 4 -2 hivyo kutwaa taji la Supercup la ufunguzi wa msimu wa Ligi Kuu ya Ujerumani.Aliibuka na kuwa mchezaji wa sita kufunga mabao matatu peke yake yaani ‘Hat Trick’ katika mchezo wake wa kwanza akiwa na Dortmund ilipocheza na Ausburg na kuifunga mabao 4 – 0.Magoli yaliendelea kutiririka huku Aubameyang akijipanga vilivyo hasa kutokana na kuzifumania nyavu mara saba katika mechi 11 alizocheza katika klabu inayofundishwa na Jurgen Klopp.Wakati soka lake kwa upande wa klabu liliendelea kukua kwa mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 24, mwaka 2013 ulikuwa si wa kuridhisha upande wa kimataifa.Hata hivyo, mwanga ulichomoza tena pale alipopachika ‘Hat Trick’ kwa njia ya penalty dhidi ya Niger katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia mnamo mwezi Juni, lakini huo ulikuwa ushindi pekee wa timu ya taifa ya Gabon maarufu kama ‘Panthers’ na kushika nafasi ya tatu katika kundi lao, hivyo kufuta matumaini ya kushiriki Kombe la Dunia litakalofanyika nchini Brazil mnako 2014.
Maoni ya wadadisi wa soka kumhusu Emerick
Mshambuliaji huyo wa Gabon alifunga ‘Hat Trick’ dhidi ya klabu ya Augsburg katika mechi ya ufunguzi ya msimu mpya na kudhiirisha moja kwa moja kwa mashabiki kwamba, alistahili kununuliwa kwa Paundi milioni 11 na kujiunga na klabu hiyo ya Ujerumani.Huo kimsingi utakuwa ulikuwa mwaka muhimu kwa mshambulijai huyo mwenye miaka 24. Mnamo mwaka 2012, alivutia katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, iliyofanyika nchini mwake na baada ye alighairi kujiunga na Tottenham Hotspur.Hivyo 2013, Aubemeyang alilazimika kudhiirisha kwamba, anaweza kufikia kiwango cha juu , na kweli alifanya hivyo .Bao lake la St Etienne, katika ushindi wa timu yake wa mabao 3 – 0 dhidi ya Bastia mnamo Januari, ulikuwa ni mwanzo wa mfululizo wa kupachika mabao ambao ulimfanya azifumanie nyavu katika mechi saba za Ligi Kuu ya Ufaransa.Aubameyang alimaliza msimu akiwa amepachika mabao 19 katika ligi, na pia alitoa pasi iliyozaa bao la ushindi katika fainali ya Kombe la Ligi la Ufaransa, baada ya St – Etienne kushinda kombe muhimu baada ya miaka thelathini.Alihusishwa na kujiunga na klabu kubwa katika majira ya jotona mengi yanasemwa kuhusu kiwango chake cha usakataji kabumbu, na kwamba, Borussia Dortmund, timu ambayo iliifunga Real Madrid ili kufikia fainali ya Kombe la Klabu Bingwa Ulaya, ilipambana vilivyo kupata saini ya mwanandinga huyo.Inawezekana Aubameyang hapangwi katika kikosi kinachoanza pale timu yake inapocheza kwa sasa, lakini Jurgen Klopp, mpishi wa mafanikio ya Dortmund, anasema tayari ameonesha mafanikio makubwa na kuvutia, katika moja ya vilabu vyenye kipaji Barani Ulaya.Moja ya mafanikio hayo ni pamoja na kufanikiwa kukimbia muda wa haraka zaidi kwa mita thelathini kuliko bingwa wa mbio za mita 100 duniani Usain Bolt.Licha ya juhudi kubwa za Aubameyang, timu ya taifa ya Gabon imeshindwa kuonesha cheche kwa mwaka 2013, lakini kwa upande wa klabu umekuwa ni mwaka wa mafanikio kwa mshambuliaji huyo.Na hivyo basi nitampigia kura kuwa Mwanasoka Bora wa Afrika wa BBC kwa mwaka 2013.Alhamisi, 21 Novemba 2013
VIJUE VIWANJA KUMI BORA NA VYENYA MWONEKANO MZURI ZAIDI DUNIANI
Namba 10
Estadio Azteca, Mexico City, Mexico
Kiwanja hiki ndicho kilichochezewa fainal ya kombe la dunia mwaka 1970 na mwaka 1986 wakati Nchi ya mexico ilipo andaa michuano hiyoo mikubwa kabisa duniani. kati ya ITALIA na BRAZIL mchezo uliomalizika kwa brazili kunyakua kombe hilo baada ya ushindi wa goli 4 - 1.Kiwanja hiki cha Azteca kina uwezo wa kubeba watazamaji wasiopungua laki moja (100,000) walioketi kwenye viti.
Kiwanja hiki kina nyasi marizawa za kupandwa katika eneo lake la kuchezea (pitch)
Namba 9
Nou Camp, Barcelona, Spain
Kiwanja hiki kinachomilikiwa na klabu ya brcelona ya Uhispania ambacho kilichezewa fainali ya klabu bingwa ya ulaya mwaka 1999 kati ya MANCHESTER UNITED na BUYERN MUNICH na manchester kutwaa ubingwa huo kwa ushindi wa goli 2 - 1. Ujenzi wa uwanja huu ulimalizika mnamo mwaka 1957 na uligharimu kiasi cha dola za kimarekani milion 3, Hadi sasa uwanja huu ndio mkubwa kuliko yote barani ulaya.Kiwanja hiki kinachukua watazamaji laki moja na ishirini elfu (120,000) walioketi kwenye viti hadi kufikia tafiti zilizofanywa na UEFA hivi karibuni
Kiwanja hiki kina nyasi maridhawa za kupandwa katika eneo lake la kuchezea (pitch) zinazowawezesha wanandinga kupiga pasi watakavyoo.
Namba 8
Old Trafford, Manchester, England
Kiwanja hiki kina milikiwa na mabingwa mara 20 wa ligi kuu ya Uingereza na mabingwa mara 2 UEFA champions league. kiwanja hiki kilikamilisha ujenzi wake na kuanza kutumiwa na man mnamo mwaka 1910.Kiwanja hiki kin uwezo wa kubeba watazamaji walioketi kwenye viti takribani elfu sabini na nane (78,000) tofauti na miaka ya nyuma wakati ulikuwa unabeba watu elfu sitini na nane (68,000).
Kiwanja hiki kina nyasi maridhawa za kupandwa katika eneo lake la kuchezea (pitch) ambazo hung'olewa na kupandwa upya kila baada ya msimu kumalizika

Namba 7
Estadio Santiago Bernabeu, Madrid, Spain
Kiwanja hiki kina milikiwa na klabu ya Real Madrid ya Uhispania. Ni kiwanja chenye historia lukuki na za kuvutia ambacho kilipewa jina na mwasisi wake Bw. Santiago Bernabeu mwaka 1953 baada ya kuhama kwenye kiwanja chao cha awali Chamartin Stadium kilichoharibiwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1924.kiwanja hiki niuwezo wa kubeba watazamaji wasio pungua elfu themanini na tano mia nne hamsini na nne(85, 454) walio keti kwenye viti.
Kiwanja hiki kina nyasi maridhawa za kupandwa katika eneo lake la kuchezea (pitch)ambazo hufanyiwa matunzo na jopo la wataalamu kutoka kitivo cha nyasi katika chuo kikuu cha hispania.
Namba 6
Louis II, Monte Carlo, Monaco
uwanja huu unamilikiwa na klabu ya AS Monaco ya Ufaransa upo pembezoni ya jiji la monaco nchini ufaransa ni moja kati ya viwanja vivutio duniani kwani kipo karbu na ukwe maarufu nchini ufarasa. kilijengwa mnamo mwaka 1937.Kiwanja hiki kina uwezo wa kubeba mashabiki takribani elfu ishirini (20,000) walioketi kwenye viti. Pamoja na udogo wa uwanja huu bado unabaki kuwa moja ya viwanja vinavyovutia zaidi duniani.
Kiwanja hiki kina nyasi maridhawa za kupandwa katika eneo lake la kuchezea (pitch) maalumu zilizoagizwa kutoka Falme za Kiarabu na Abu Dhabi
Namba 5
San Siro, Milan, Italy
Kiwanja hiki kina milikiwa na klabu mbili hasimu zaidi nchini Italia AC Milan na Inter Milan. Katika uwanja huu kila kitu ni kandanda, kabumbu, mpira au soka ni moja kati ya vuwanja vyenye historia kubwa duniani. Mashabiki wendawazimu wa soka wanapatikana kaika dimba hilo.
Kiwanja hichi kilijengwa na uwezo wa kubeba mashabiki elfu themanini (80,000) walio kaa kwenye viti hivyo hauna barabara za kukimbilia kuuzunguka uwanja
Kiwanja hiki kina nyasi maridhawa za kupandwa katika eneo lake la kuchezea (pitch)
Namba 4
Maracana, Rio De Janeiro, Brazil
Kiwanja hiki kinamlikiwa na timu ya taifa ya Brazili ni moja kati ya viwanja bora na vyenye mvuto wa kipekee duniani. Ndio uwanja uliowahi kuingiza watazamaji wengi zaidi duniani takribani 200,000 kwenye fainali za kombe la dunia mwaka 1950, Huku brazili akiwa mwenyeji. Kiwanja hiki kilijengwa maalumu kwaajili ya michuano ya mwaka 1950 na kiligharimu dola za kimarekani milioni 40.Kiwanja hichi kina uwezo wa kubeba watazamaji laki moja ishirini na tano elfu (125,000) waliokaa kwenye viti na watazamaji zaidi ya elfu thelathin na moja mia saba arobaini (31,740) waliosimama.
Kiwanja hiki ina nyasi asilia za kupandwa zilizokatwa kwa mtindo wa drafti katika sehemu ya kuchezea (pitch).
Namba 3
Stadio Olimpico, Rome, Italy
Kiwanja hiki kinachomolikiwa na AS Roma awali kilijengwa kwaajili ya mashindano ya olimpiki mwaka 1960 ila baada ya hapo kilionekana kinafaa kwaajili ya michezo ya soka hasa baada ya kujengewa paa la juu na mara kadhaa umetumika kwenye mechi za timu ya taifa ya Italia.Kiwanja hichi kina uwezo wa kubeba watazamaji Elfu themanini na mbili na mia tatu (82,300) waliokaa kwenye vit.
Kiwanja hiki kina nyasi asilia za kupandwa katika eneo la kuchezea (pitch) ambazo zimekatwa kwa mtindo wa kuzunguka sehemu ya katikati ya kiwanja.
Namba 2
Azadi, Tehran, Iran
Linaweza kwa jambo la kushangaza katika medani ya soka juu ya nchi kama Irani kumiliki moja kati ya viwanja bora kabisa vya soka duniani lakini ndo hali halisi kiwanja hiki cha Azadi kijitengenezwa mwaka 1974 kwaajili ya michuano ya bara la Asia .kiwanja hiki kina uwezo wa kubeba watazamaji wasiopungua laki moja na ishirin (100,020) walioketi kwenye viti na zaidi ya idadi ya elfu thelathini (30,000) waliosimama
Kiwanja hiki kina nyasi asilia za kupandwa katika eneo lake la kuchezea (pitch) ambazo zimekatwa kwa mtindo wa mistari sambamba ambayo unauongezea unadhafu uwanja huo.
Namba 1
International Stadium Yokohama, Yokohama, Japan
Kiwanja hiki ndicho kilichochezewa fainali ya kombe la dunia mwaka 2002 kati ya Ujerumani na Brazili. kiwanja hiki hadi kukamilika kwake kiligarimu Yen bilioni 60 na ndicho kiwanja kikubwa zaidi nchii Japani.Kiwanja hiki kinauwezo wa kubeba watazamaji walioketi kwenye viti elfu sabini (70,000)
Kiwanja hiki kina nyasi asilia za kupandwa katika eneo la kucheea (pitch) ambazo haziwezi kukauka katika kipindi cha kiangazi maana nchini ardhini zimetandazwa bomba maalumu kwaajili ya kutoa mvuke utakaoendeleza ukuaji wa kiwanja hicho.
Je unadhani list hii ipo sahihi toa maoni yako na wewe na list yako nasi tutaitolea ufafanuzi na kuibandika kwenye blog yetu hii.
Jumatatu, 18 Novemba 2013
TAIFA STARS KUCHEZA NA ZIMBABWE NA SI KENYA KAMA ILIVYORARAJIWA
Taifa Stars sasa inacheza na Zimbabwe mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu Fifa Date itakayofanyika Novemba 19 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Awali Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ilikuwa icheze na Kenya (Harambee Stars), lakini Shirikisho la Mpira wa Miguu Kenya (FKF) lilituma taarifa jana jioni (Novemba 16 mwaka huu) likieleza kuwa timu yake haitacheza tena mechi hiyo.
Kikosi cha Zimbabwe chenye msafara wa watu 30 kinatarajia kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kesho (saa 3 asubuhi) tayari kwa mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 11 kamili jioni.
Waamuzi wa mechi hiyo wanatoka Uganda wakati Kamishna atakuwa Leslie Liunda wa Dar es Salaam. Mwamuzi wa mezani ni Oden Mbaga pia wa Dar es Salaam.
Stars chini ya Kocha Kim Poulsen ipo kambini tangu Novemba 12 mwaka huu kujiwinda kwa mechi hiyo. Kim amejumuisha kwenye kikosi chake wachezaji watano wanaocheza mpira wa miguu nje ya Tanzania.
Kiingilio katika mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya wenyeji Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe ni sh5,000 wakati tiketi zitaanza kuuzwa Jumatatu (Novemba 18 mwaka huu) kwenye vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Mbali ya kiingilio hicho cha sh5,000 ambacho ni kwa viti vya bluu na kijani, viingilio vingine ni sh30,000 kwa VIP A, sh20,000 kwa VIP B, sh15,000 kwa VIP C wakati viti vya rangi ya chungwa ni sh10,000.
Tiketi zitauzwa katika magari maalumu katika vituo vya; Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa Ohio na Samora, Sokoni Kariakoo, Dar Live Mbagala, OilCom Ubungo, BMM Salon iliyopo Sinza Madukani, Uwanja wa Uhuru, mgahawa wa Brake Point uliopo Kijitonyama, na kituo cha mafuta Buguruni.
Jumapili, 17 Novemba 2013
VIJANA CHINI YA MIAKA 17 NIGERIA WANAVYOTAKATA KWA MADOLA
Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria amewazawadia Kiasi
cha Dola 12,600 kila mchezaji,wachezaji wote wa Timu ya Taifa soka
Nigeria ya chini ya umri wa miaka 17,ikiwa ni zawadi kwa Kutwaa Ubingwa
wa soka wa Dunia mwishoni mwa wiki iliyopita,
Wachezaji hao walitwaa Ubingwa wa Dunia kwa kuilaza Mexico bao 3-0 Ijumaa iliyopita mjini Abudhabi.Rais Goodluck Jonathan pia aliahidi kutoa nishani za kitaifa kwa viongozi wa timu timu hiyo huku akiagiza wadau mbali mbali kutoka sekta binafsi kumuunga mkono katika kuizawadia Timu hiyo.
Katika Mapokezi ya Timu hiyo Mjini Abuja,Rais Jonathan alisema Huu ni ushindi wenu halali na wa kujivunia.
Kiongozi huyo aliendelea kusema kuwa Ushindi huo wa Vijana ni mwanzo mpya wa kufufua moyo wa ushindani nchini Nigeria.
Katika Kipindi cha Miezi saba Timu hii imetoka nafasi ya pili kwa ubora barani Afrika hadi kuwa nafasi ya kwanza kwa ubora duniani.
Mwaka 2007,aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Umaru Yar’adua aliwazawadia kila mchezaji nyuma ya vyumba vitatu baada ya kutwaa Ubingwa wa Dunia kwa wachezaji wa umri chini ya miaka 17 nchini Korea Kusini.
Wachezaji hao pia walizawadiwa nishani ya juu ya heshima nchini Nigeria kutokana na ushindi huo.
Rais Jonathan ametoa wito kwa shirikisho la soka la Nigeria NFA kuwaendeleza vema wachezaji hao ili hatimaye waweze kuichezea Timu ya taifa ya wakubwa ya Nigeria Super Eagles.
Hata Hivyo Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Nigeria Steven Keshi amesema si vema kuwalazimisha wachezaji hao kuichezea Timu ya taifa ya wakubwa.
Kocha huyo ambaye pia aliwahi kuwa nahodha wa Timu ya taifa ya soka ya Nigeria alisema kuwa binafsi angependelea wachezaji kufuata njia ya kawaida na kukua kiuchezaji ili wachezee timu ya umri chini ya miaka 20 na 23 na hatimaye ndipo waweze kupandishwa kuchezea kikosi cha Super Eagles hususan kwa wale watakaokuwa wameonyesha uwezo mkubwa.
Hii ni mara ya nne kwa Timu ya taifa ya Nigeria chini ya umri wa miaka 17 kutwa Ubingwa wa Dunia baada ya kufanya hivyo mwaka 1985 nchini China,Mwaka 1993 nchini Japan,2007 korea kusini na mwaka huu 2013 Falme za Kiarabu.
Alhamisi, 14 Novemba 2013
HUU NI UCHAMBUZI WA GWIJI WA ZAMANI WA NIGERIA SUDAY OLISEH JUU YA NANI BORA KATI YA MESSI NA RONALDO
Kama unakabiliwa na uchaguzi,juu, ya nani anastahili kuwa wa Mchezaji bora wa Dunia wa Mwaka,kati nyota hawa wawili Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wewe unadhani ni nani anayestaili tuzo hiyoo? Kumekuwa na utata mkali sana kuhusiana na wachezaji hawa bora zaidi kwa sasa ulimwenguni utajaribu kutathmini uwezo wao katika idara kadhaa ya mchezo.
Je? Lionel Messi amepoteza sifa za kuwania tuzo ya mchezaji bora wa dunia mwaka huu?
Je? Cristiano Ronaldo Amefanya yanayostaili kushinda tuzo hiyo mwaka huu kutokana na kiwango chake?
Tafadhali kumbuka maneno muhimu hapa. Sisi tunatathmini sifa zao ndani ya uwanja wa mpira-kuhusiana utendaji, na siinje ya uwanja ubishi au hisia.
Messi:- Katika utawala wa koch Pep Guardiola Messi alikuwa ni mchezaji mwenye kasi zaidi ambaye sijawahi mwona anapokuwa na mpira kwenye miguu yake ni mwepesi wa kukimbia anapokuwa na mpira vile vile asipokuwa nao ni mwepesi wa kufika maeneo mpira ulipo. Messi amekuwa akizinyanyasa safu mbalimbali za mabeki pindi anapokuwa na mpira vile vile kupiga chenga pale anapokuwa na mpira na kwa kasi ile ile
Ronaldo:- ukitaka kujua Ronaldo yupo kasi kiasi gani ni vema atazamwe akiwa anacheza uwanjani huwa anakimbia kwa kasi ya ajabu ambayo huwaacha mabeki wa timu pinzani wasijue nin cha kufanya. Pamoja na hayo Ronaldo anahitaji nafasi anapokuwa uwanjani ili aonyeshe kasi yake tofauti na Messi ambaye wakati wowote anaweza kufanya tukio lolote. Vile vile Ronaldo ni mrefu kuliko Messi jambo ambalo humwongezea kasi.
NAFASI YA ULINZI
Kwa soka la kisasa linamtaka kila mchezaji awapo uwanjani asaidiane na safu ya kiungo pamoja na beki ili kuimarisha usalama wa timu.
Mara nyingi Messi amekuwa ni mchezaji hatari tu pale anapokwenda kushambulia na si kufanya ulinzi kwa timu ya ke hususani kurudi hadi nusu ya eneo la timu yake . ila inaeleweka kwamba Barcelona wanamiliki mpira kiasi cha asilimia 65 hivyo mara nyingi haimuhitaji messi kurudi kusaidia kwenye ulinzi wakati timu inashambuliwa
Kwa namna Ronaldo anvyosaidia safu yake ya ulinzi katika klabu ya Real Madrid inavutia kwa sababu si tu anarudi hadi eneo la timu yake bali hurudi kuzuia faulo na mipira mingine ya adhabu kama kona. Kusaidia kwake kukaba kwa nguvu ni sababu tosha inayomtofautisha na mpinzani wake kwasababu Ronaldo hupata Kadi za njano sana
UPIGAJI WA MASHUTI LANGONI MWA ADUI
Ronaldo ni nzuri katika idara hii yeye hupiga mashuti, ambapo mpira inakuwa na speed ajabu lakini ufanisi huu huwachanganya sana makipa. Kila msimu, yeye uwa anafunga magoli hayo kutoka umbali mkubwa na zoezi hili hulifanya kwa ufanisi mkubwa kwa kutumia miguu yote miwili.
Messi yeye hupendelea kuachia mashuti makali karibu na lango pia hutegemeana na ni kwa jinsi gani nafasi imepatikana kitu ambacho hakionyeshi uhalisia wa uwezo alio nao.
Mara nyingine tena tahadhari lazima kutekelezwa hapa kama mtindo wa Barcelona kucheza ya "Tiki Taka" hivyo humfanya mesi afunge magoli akiwa umbali mdogo
UMILIKAJI MPIRA NA MBINU BINAFSI
Kama duniani kungekuwa na wachezaji wenye sifa ya kuwa na sifa ya umilikaji wa mpira wa miguu basi hao si wengine bali ni Cristiano Ronaldo na Lionel Messi
Ronaldo anaonekana kuwa ni mchezaji ambaye anaweza kuuamrisha mpira ukafuata anachotaka yeye hata baadhi ya video zake kwenye mtandao wa You Tube zinadhihirisha hilo
Messi anautaalamu pale anapokuwa anamiliki mpira kwenye miguu yake anaweza kikimbia kitoka upande mmoja kwenda mwingine na kuwapita walinzi hata mahali ambapo hapatarajiwi yeye kupita.
UTIMAMU WA MWILI
Lionel Messi aliwahi kucheza mechi 25 za Barcelona bila kukosa hata moja hiyo yote isisaidiwa na utimamu wa mwili (physical fitness ) itimamu wake wa mwili ulimsaidia kupambana na majeraha kidogo aliyokuwa anakumbana nayo kutoka kwa walinzi wa timu fulani.
Cristiano Ronaldo ni hivyo hivyo yeye anafaa kwamba yeye anafaa kwaajili ya matangazo ya chupi na inajulikana kuwa mpenda vimwana sana ingawa, kutokana na sura yake ya kuvutia, wakosoaji kushindwa kuona au kukubali kwamba yeye pengine ni mchezaji aliefit zaidi katka dunia ya leo.
MAGOLI
2013 takwimu za mabao ni wazi zinaegemea upande wa Ronaldo. Messi imejitahidi kukaa vizuri kutokana na ya kifundo cha bega nimeongeza na, kama vile, yeye amekosa michezo muhimu mwaka huu. Ronaldo bado hasakosa mchezo kutokana na majeruhi.
MCHEZAJI WA TIMU
katika hali ya kawaida Messi huonekana yupo kitimu zaidi hata akifunga goli hushangilia na wezake zaidi ya Ronaldo ambaye yeye yuko kibinafsi zaidi.
Ni vigumu kujua kwamba Messi anacheza kwenye timu ambayo wachezaji wote macho yao yameelekezwa kwake na ndio sababu kubwa ya kushangilia huku akiwashukuru wezake AU ni sabau inayomfanya Ronaldo ajihisi yupo peke yake maana hufunga baadhi ya magoli bila msaada wa wenzake?
Ni vigumu kung'amua swali hili.
MSHINDI
Kwa maoni yangu nadhani Frank Ribery ndiee mchezaji bora na aliyekamilika kwa kila kitu sasa hapa duniani
Je? Unadhani anastahili tuzo hii?
JE WAYAJUA MAMBO HAYA 5 MUHIMU USIYOYAJUA KUHUSU AMBAYO MCHAWI WA SOKA BRAZILI EDSON ARANTES DO NASCIMENTO "PELE"
Mwanasoka anayedhaniwa na shirikisho la soka duniani (FIFA) kuwa bora na wa muda wote EDSON ARANTES DO NASCIMENTO "PELE" amekuwa akijadili mafanikio yake mara kwa mara na hasa wakati linapokuja suala la kumlinganinisha na staa mwenzake wa zamani wa imu za Palemo, Napoli, Boca Jounior, na timu ya taifa ya Argentina DIEGO ALMANDO MARADONA kwamba nani bora yapo mambo matano yaliyofichika juu ya mafanikio yake kupitia mitandao ya kijamii hasa wa selict tumeweza kugundua haya
He even counted games he played for the Sixth Coast Guard in the military competition.
He officially scored 757 goals in 812 games.
As great as Pelé's goal scoring ratio was, it pales in comparison to Fernando Peyroteo.
Of course, Pelé probably would dismiss Peyroteo's achievements, just like I'm about to dismiss some of the Brazilian's goals.
Looking through Emilio Castaño's statistical analysis of Pelé's goal-scoring feats, you can't help but notice irregularities.
Scoreline Pelé's goals
Santos 11-0 Botafogo Ribeirão Preto 8
Santos 11-1 Maringá 5
Santos 10-3 Nitro-Química 5
Santos 10-0 Nacional 5
Santos 10-1 Royal Neerschot 5
Santos 10-2 Guarani 5
Santos 10-1 Juventus 5
The eight goals Pelé scored against Botafogo didn't come against the Botafogo.
5. Pelé Didn't Officially Score 1,283 Goals
Pelé did score 1,283 goals, but 526 goals came in unofficial friendlies and tour games.He even counted games he played for the Sixth Coast Guard in the military competition.
He officially scored 757 goals in 812 games.
As great as Pelé's goal scoring ratio was, it pales in comparison to Fernando Peyroteo.
Of course, Pelé probably would dismiss Peyroteo's achievements, just like I'm about to dismiss some of the Brazilian's goals.
Looking through Emilio Castaño's statistical analysis of Pelé's goal-scoring feats, you can't help but notice irregularities.
Scoreline Pelé's goals
Santos 11-0 Botafogo Ribeirão Preto 8
Santos 11-1 Maringá 5
Santos 10-3 Nitro-Química 5
Santos 10-0 Nacional 5
Santos 10-1 Royal Neerschot 5
Santos 10-2 Guarani 5
Santos 10-1 Juventus 5
It came against a side bearing the same name and whose only achievement was producing the late great Sócrates.
It's not the Uruguayan Nacional but some state side in São Paulo. The same applies to Juventus—not the European one, but another irrelevant state side.
Using a modern-day example, it's like Chelsea beating up on Brentford and Leyton Orient in a separate London league.
Even Fernando Torres would score goals against those sides.
A real gauge of Pelé's goal-scoring ability was his international record.
He never scored four goals or more in a game and his 77 goals in 92 games is mortal, as opposed to his mythical 1,283 goals.
4. A Reality Check
Pelé needs a reality check regarding his FIFA World Cup achievements.
Most World Cup All-Star appearances Djalma Santos and Franz Beckenbauer, 3
Most World Cup goals Ronaldo, 15
Most World Cup goals in one final Geoff Hurst, 3
Most World Cup goals in one tournament Just Fontaine, 13
Most World Cup goals in one game Oleg Salenko, 5
Most World Cup games Lothar Matthäus, 25
Most World Cup games won Cafu, 16
Most World Cup tournaments Antonio Carbajal and Lothar Matthäus, 5
Where's Pelé?
3.Pelé Was Outperformed in Every Single World Cup
Pelé played in four FIFA World Cup tournaments but was outperformed in every single one of them.
For a man that boasts about his goal-scoring prowess, I find it amusing that he never mentions himself as a Silver Boot winner.
Year Golden Boot Winner,goals Pelé's goals
1958 Just Fontaine, 13 6
1962 Six players tied, 4 1
1966 Eusébio, 9 1
1970 Gerd Müller, 10 4
To be fair, Pelé was injured during the 1962 and 1966 World Cup. When he was fully fit for the 1958 and 1970 World Cup, he wasn't the top goal scorer.
In fact, he wasn't even Brazil's top scorer during the 1970 World Cup. That accolade went to Jairzinho with seven goals.
2.Pelé Won Two FIFA World Cups, Not Three
Here's Pelé laying down the gauntlet to Lionel Messi: People always ask me: "When is the new Pele going to be born?" Never. My father and mother have closed the factory. When Messi's scored 1,283 goals like me, when he's won three World Cups, we'll talk about it.
Messi needs to reach 758 goals instead of 1,284 and needs to win two FIFA World Cups instead of three.
Pelé was a member of three World Cup-winning teams, but he sat out the large majority of the 1962 World Cup.
It was Garrincha who singlehandedly won the World Cup for Brazil, not Pelé.
1. Pelé Played with Historic Teammates
When Pelé compiled his 125 greatest living footballers list, he didn't include many of his teammates.
Regarding the teammates that made the cut: There are two of the greatest right-backs ever in Carlos Alberto and Djalma Santos. Then there is one of the greatest left-backs ever in Nílton Santos. Also a marvelous midfielder in Rivelino.
Here are Pelé's teammates who were ineligible for his list: Garrincha (inspired Brazil to win the 1962 FIFA World Cup), Vavá (scored three goals in two World Cup finals) and Didi (1958 World Cup Golden Ball winner).
Pelé shockingly omitted teammates: Gérson, Jairzinho, Gilmar, Tostão, Zito, Bellini and Zagallo.
I read into the omissions as Pelé's way of downplaying his teammate's role in his success.
I would have liked to see Pelé symbolically include Santos strike partner Coutinho on the list as a way of saying thank you. After all, they did supposedly combine for over 1,000 goals.
I'll never forget what Gérson, who was Pelé's Xavi, said this about his role in that legendary 1970 World Cup team:
Now the interesting thing is this, as incredible as it might seem, I prefer a thousand times over to make the pass, rather than to score the goal. For me this was the glory because this is what I was trained for.
It was disgraceful that Pelé forgot about the thousands of passes Gérson made.
Meanwhile, Lionel Messi dedicated his FIFA Ballon d’Or to Xavi: "I want to share this with my friend, he deserves it."
Has anyone ever wondered were Pelé was when Garrincha's life was spiraling out of control?
Never forget that Pelé played with historic teammates who made him into the living legend he is.
They were that good that they didn't even need Pelé for the 1962 World Cup.
Jumatano, 13 Novemba 2013
KAPOMBE AANZA KUIONA TAMU YA KUCHEZA SOKA ULAYA
Hatimaye nyota na beki mahiri wa kimataifa wa tanzania SHOMARI KAPOMBE aanza kunyookewa na mambo baada ya hapo juzi kupiga picha na moja kati ya mabeki mahiri alietamba katika soka la ulaya WILLIUM GALLAS aliyengara na vilabu kama Chelsea, Arsenal an Tottenham Spurs za Uingereza na sasa ameamua kurudi nyumbani kufanya mazoezi na clab ya AS Cannes. Kapombe mwenyewe amefurahishwa na hatua hiyo huku akisema atajifunza mambo mengi sana kutoka kwa beki huyo wa kati wa zamani wa timu ya taifa ya UFARANSA "Imekuwa ni faraja kwangu kukutana mtu kama Willium Galllas na kubwa zaidi kufanya nae mazoezi natumaini ntajifunza mambo mengi kutoka kwa mchhezaji huyu kutokana na uzoefu wake," Kwa upande mwingine Gallas ameelezea kufurahiswa na kiwango cha nyota huyo wa zamani wa simba na kusema kuwa atakuja kuwa moja kati ya malinzi mahiri duniani kama ataendelea na juudi alizonazo
"Actually i have been impressed by his performance, and i think he may become a great player if he keeps on his effort. He is a good player general "
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)