Jumamosi, 19 Oktoba 2013

ZIJUE KLABU KUBWA NA MAARUFU ZA SOKA ZAIDI DUNIANI

(10) JUVENTUS
Juventus: Juventus ni kabu ya soka inayoshiriki ligi kuu ya nchini italia kwa sasa imewekwa katika nafasi ya 10 katika orodha ya klabu maarufu zaidi duniani kwakuwa na mashabiki milioni 21 duniani kote.Hii inatokana kufanya vizuri katika michuano mbalimbali iikiwamo kuchukua kombe la ligi kuu nchini itali ikiwa ni pamoja na kufika hatua ya robo fainali ya ligi ya klabu bingwa ulaya ( U.E.F.A) msimu wa 2012/2013

(9)INTER MILAN
Milan Inter: Inter Milan  ni kabu ya soka inayoshiriki ligi kuu ya nchini italia inatua katika nafasi ya 9 inatarajiwa kuwa na mashabiki milioni 24 duniani kote kwa sasa hii ni kutokana na kuwa moja ya klabu kongwe barani ulaya zilizojizolea mashabiki wengi  duniani kote hususani kipindi ambacho ilikuwa chini ya kocha anayeaminika kuwa kocha wa kipekee (Special One) Jose Mourinho

(8)BAYERN MUNICH

Munich Bayern: Bayern  ni kabu ya soka inayoshiriki ligi kuu ya nchini Ujeruman inakadiriwa kuwa na mashabiki milioni 50 duniani kote ambao inawafanya kushika nafasi ya 8 katika orodha ya klabu maarufu zaidi za mpira wa miguu.  Hii imetokana na kufanya kwake vizuri katika ligi ya BUNDESLIGA pamoja na michuano ya U.E.F.A kwa msimu wa mwaka 2012/2013

(7)LIVERPOOL

Liverpool: Liverpool  ni kabu ya soka inayoshiriki ligi kuu ya nchini Uingereza pamoja na kutokufanya kwake vizuri katika michuano mbali mbali bado imeendelea kuwa klabu mashuhuri yenye mashabiki wengi wanaokadiriwa kufikia milioni 70 duniani kote hadi hivi sasa hvyo inashika nafasi ya  7 kwa kuwa klabu maarufu zaidi duniani
(6)AC MILAN
Ac Milan: Milam ni kabu ya soka inayoshiriki ligi kuu ya nchini italia kwa sasa imewekwa katika nafasi ya 6 katika orodha ya klabu maarufu zaidi duniani kwakuwa na mashabiki milioni 98 duniani kote.Hii inatokana kufanya vizuri katika michuano mbalimbali iikiwamo kushika nafasi nne(4) za juu kwenye ligi ya italia hivyo kupata nafasi ya kushiriki ligi ya klabu bingwa ulaya ( U.E.F.A) msimu wa 2013/2014





(5)ARSENAL

Arsenal: Arsenal  ni kabu ya soka inayoshiriki ligi kuu ya nchini Uingereza pamoja na kutokufanya kwake vizuri katika michuano mbali mbali bado imeendelea kuwa klabu mashuhuri yenye mashabiki wengi wanaokadiriwa kufikia milioni 115 duniani kote hadi hivi sasa hvyo inashika nafasi ya  5 kwa kuwa klabu maarufu zaidi duniani na inasadikika mashabiki wengi wa klabu hii wanapatikana katika mabara ya Asia na Afrika

(4)CHELSEA
Chelsea: Chelsea  ni kabu ya soka inayoshiriki ligi kuu ya nchini Uingereza amayo kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa ikifanya vizuri katika michuano mbali mbali na imeendelea kujikusanyia mashabiki wengi wanaokadiriwa kufikia milioni 140 duniani kote hadi hivi sasa hvyo inashika nafasi ya 4 kwa kuwa klabu maarufu zaidi duniani

(3)REAL MADRID

Real Madrid: Real  ni kabu ya soka inayoshiriki ligi kuu ya nchini Hispnia imekuwa ni klabu inayofanya vizuri kwa muda mrefu sasa na kinachovutia watu wengi duniani ni mpango wa klabu hiyo kusajili wachezaji wote maarufu duniani kama Ronaldo De Lima, David Beckham, Luis Figo, Zinedine Zidane jambo ambalo limewaongezea mashabiki wengi wanaokadiriwa kufikia milioni 180 duniani kote hadi hivi sasa hvyo inashika nafasi ya 3 kwa kuwa klabu maarufu zaidi duniani

(2)BARCELONA

Barcelona: Barca  ni kabu ya soka inayoshiriki ligi kuu ya nchini Hispnia imekuwa ni klabu inayofanya vizuri kwa muda mrefu sasa na kinachovutia watu wengi duniani ni mpango wa klabu hiyo kukuza wachezaji na kucheza soka maridhawa huku kivutio kikubwa kikiwa ni nyota wake wa kiargentina Lionel Messi  jambo ambalo limewaongezea mashabiki wengi wanaokadiriwa kufikia milioni 260 duniani kote hadi hivi sasa hvyo inashika nafasi ya 2 kwa kuwa klabu maarufu zaidi duniani


(1) MANCHESTER UNITED

Manchester United: Man u  ni kabu ya soka inayoshiriki ligi kuu ya nchini Uingereza pamoja na kutokufanya kwake vizuri katika msimu huu wa ligi ya EPL bado imeendelea kuwa klabu mashuhuri yenye mashabiki wengi wanaokadiriwa kufikia milioni 350 duniani kote hadi hivi sasa hvyo inashika nafasi ya  1 kwa kuwa klabu maarufu zaidi duniani na inasadikika mashabiki wengi wa klabu hii wanapatikana katika mabara ya Asia na Afrika







Hakuna maoni:

Chapisha Maoni