Rais wa TFF, Jamal Malinzi ameutolea ufafanuzi mgogoro wa Simba unaoendelea hivi sasa baada ya mwenyekiti wa Simba Ismail Aden rage kupinga agizo la kuitisha mkutano wa wanachama ndani ya siku 14 ambazo zinaisha Desemba 6. Malinzi ametaja hatua zitakazochukuliwa pale siku hizo zitakapoisha. Tazama video hii kufahamu zaidi
Alhamisi, 5 Desemba 2013
Jumatatu, 2 Desemba 2013
AZAM TV KUANZA KURUSHA MATANGAZO YAO KUANZIA DEC 6 MWAKA HUU
KAMPUNI ya Azam Media imezindua rasmi kituo cha televisheni ya Azam TV
‘Burudani kwa Wote’ ambacho kitaanza kuwa hewani kuanzia Desemba 6, mwaka
huu.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam
Media, Rhys Torrington, alisema matangazo hayo yatakuwa yakipatikana
Tanzania nzima na nchi nyingine za Afrika Mashariki kwa kutoa burudani na
vipindi mbalimbali.
Alisema kituo hicho kitakuwa na huduma kutoka chaneli 50 zikiwemo za
kimataifa, za ndani ya Tanzania na tatu kutoka Azam zitakazorusha matangazo
ya Kiswahili, kimataifa na filamu za Kitanzania.
“Kwa kutazama michezo, sinema na matangazo mbalimbali ya miundo ya maisha
mteja wetu atakuwa akilipia sh 12,500 kwa mwezi ili kupata matangazo yetu
kwa ubora na muonekano mzuri,” alisema Torrington.
Torrington alisema kituo hicho kitakuwa kikirusha moja kwa moja Ligi Kuu ya
Bara kupitia chaneli maalumu na kuandaa vipindi mbalimbali kupitia
watayarishaji wake.
Aliongeza kuwa Azam Media iko mbioni kuanzisha kituo cha radio cha Azam FM.
Naye mgeni rasmi katika uzinduzi wa kituo hicho, Naibu Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, mbali ya kuipongeza
familia ya Bakhressa kuwekeza katika teknolojia ya utangazaji, alisema
hatua hiyo inadhihirisha Tanzania kuwa mstari wa mbele Afrika katika
mabadiliko ya urushaji wa matangazo ya televisheni kutoka analojia kwenda
dijitali kwa haraka.
Makamba alisema serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa Azam Media na
kuzidi kubuni sera nzuri zitakazoongeza uwekezaji katika sekta ya
utangazaji.
Aidha, alitoa changamoto kwa vijana wa Kitanzania wenye vipaji, kuitumia
fursa ya Azam TV kuandaa programu zao na kujiongezea kipato badala ya kukaa
kulaumu na kutuhumu.
RATIBA YA MAKUNDI KOMBE LA DUNIA 2014 KUPANGWA IJUMAA HII
MACHO na masikio ya mamilioni ya mashabiki wa soka Ijumaa hii yatahamia katika kiota cha Costa do Sauipe kilichopo katika jimbo la Bahia nchini Brazil kushuhudia upangwaji ratiba ya michuano ya Kombe la Dunia 2014. Shirikisho la Soka Duniani-FIFA limetenga kiasi cha dola milioni nane kwa ajili ya shughuli hiyo itakayoonyeshwa dunia nzima kwa dakika 90 huku ikishirikisha nyota wa soka wa Brazil pamoja na muziki utakaowapa ladha mashabiki. Baadhi ya nyota wa zamani katika soka wakiwemo Pele, Zinedine Zidane na Lothar Matthaeus watakuwepo kusaidia uapngwaji ratiba hiyo wakati maofisa 5,000, waandishi wa habari na wageni waalikwa watakuwa wakishuhudia tukio hilo muhimu. Brazil imesubiri kwa miaka 64 kuandaa michuano hiyo baada ya kushindwa kunyakuwa kombe hilo mwaka 1950 katika mchezo wa fainali dhidi ya majirani zao Uruguay katika Uwanja wa Maracana jijini Rio de Janeiro.
TUZO ZA BBC 2013 || YAYA TOURE BORA ZAIDI AFRIKA
Mchezaji huyo wa Ivory Coast, na ambaye pia ni kiungo wa klabu ya Manchester City ya Uingereza, na ambaye jina lake limekuwepo kwa miaka minne iliyopita katika orodha ya wachezaji wanaowania tuzo, aliwashinda Pierre-Emerick Aubameyang, Victor Moses, John Mikel Obi na Jonathan Pitroipa, katika kuibuka mshindi.
Mchezaji huyo ana umri wa miaka 30.
Orodha fupi ya waliowania tuzo hiyo ilitayarishwa na wataalamu 44 wa soka kutoka kote barani Afrika, na wakizingatia hasa maarifa ya mchezaji, kiufundi, ushirikiano na wenzake katika timu, na kwa kucheza mchezo safi na kwa haki.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)